Wednesday, April 1, 2015

MTANZANIA WA KWANZA KUTOA NADHARIA YAKE

Tumezoea kuona na kusikia miaka yote wagunduzi, wafumbuzi na wanasayansi mahiri dunia kama wakina Sir. Isaac Newton huwa wanatokea nchi za magharibi na bara la Asia hasa katika masuala ya taaluma ya Sayansi upande wa Fizikia na sio Afrika na kuperekea hata baadhi ya wanafunzi wenye ndoto za kugundua theori katika stadi hiyo kukata tamaaa na kudhani kuwa wazungu tu ndio wenye uwezo wa kufanya uvumbuzi. Kwasasa changamoto hiyo nadhani imefikia tamati baada tu ya Bwana mmoja aitwa Erasto Barthlomeo Mpemba kuvuma na theori yake ya "Mpemba Effect" na hatimaye kufanikiwa kuweka maswali mengi kwenye vichwa vya wanasayansi wengi na mahiri duniani na kuleta changamoto kubwa pia kwa wanasayansi hao na katika nyanja hiyo kiujumla baada kufanyika mikutano mingi juu ya theori hiyo ya "Mpemba Effect" inayosema kwamba "Maji ya moto yaliyochemka kwa kwa jotoridi la 100 centigredi, yanaganda mapema kuliko maji ya baridi" UVUMBUZI NA HISTORIA YAKE KI UJUMLA: Erasto Barthlomeo Mpemba mzaliwa wa mwaka 1950, mnamo mwaka 1963 akiwa anasoma kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Magamba Mkoani Tanga siku moja akiwa katika darasa mapishi waliagizwa kutengeneza Ice cream (Barafu tamu) ambazo zinatakiwa kuwa na mchanganyiko wa maji, maziwa na sukari na wakishamaliza waweke kwenye jokofu kwa ajili ya kugandisha, basi wakawa wanafanya hivyo na ice cream hizo zilikuwa zikiganda na kuwa barafu. Lakini siku moja waliambiwa tena wafanye zoezi hilo kwakuwa kulikuwa na uhaba wa nafasi katika jokofu hilo linalotumika kugandishia kwahiyo walikuwa wanafanya mtindo wa wakwanza kuingia wakwanza kutoka na kwa bahati mbaya siku mwenzake akataka awahi kabla basi Mpemba alichofanya ni kuruka hatua ya kupooza maziwa kabla ya kuingiza kwenye jokofu yeye aliweka hivyo hivyo bila kuhofu pengine angeharibu jokofu lakini kamari aliyoicheza alikuta kuzaa matunda tena zaidi ya alivyo fikiri kwa kuwa ilipofika muda kufunua jokofu ice cream zake ziliganda sana na wenzake zilikuwa nzito tu kama ugali lakini sio ngumu. Na tokea hapo akagundua kuwa kimiminika cha moto kinaganda mapema sana ukilinganisha na cha baridi ukivigandisha kwenye jokofu kwa pamoja. Na baadae akawa maarufu sana pale mkoani Tanga wa kuwa watengeneza ice cream wote walitumia kanuni yake ili kuokoa gharama za umeme kwa kuwa ukitumia maji au maziwa ya moto kutengenezea ice cream zinaganda mapema na zinakuwa tayari kwa kuuza. Baadae alifaulu mtihani wa kumaliza Kidato Cha Nne na akaenda Shule ya Sekondari ya Mkwawa kwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita huko Mkoani Iringa ndipo mwali mkuu alipomualika Profesa Denis Osborne kutoka chuo Kikuu Cha Dar - es - salaam (UDSM) kufindisha kipindi cha Fizikia katika darasa la sayansi na mara tu baada ya kufundisha aliamua kutoa fursa ya mwanafunzi yeyote kuuliza swali lolote, maswali yalikuwa mengi kama "utaweza kuingia chuo kikuu?", "je masomo ya sayansi ya mahusiano gani maendeleo?" ila swali ambalo lilibaki kichwani mwa Profesa ni lile alilouliza mpemba kutoka na kilichomtokea kwenye ugandishaji wa ice cream na akauliza hivi "Ukichukua maji ukaweka kwenye vyombo vyenye ujazo sawa, chombo kimoja ukaweka maji yenye jotoridi la 35 centigredi na kingine yenye maji ya jotoridi 100 centigredi na ukiviweka vigande kwenye jokofu kwa chenye jotoridi 100 centigredi huganda haraka?" Na aliendelea kunukuu "siku moja katika somo la fizikia katika maada ya Kanuni za Newton's za Upoozaji alimuuliza mwalimu kwanini maziwa ya moto na baridi ukiweka kwenye jokofu, ya moto huwai kuganda mapema? mwalimu alisema; sidhani kama inawezekana, mpemba; aliendelea kuuliza nishajaribu yanaganda ya mapema ya moto. Mwalimu akasema " Hiyo ni mpemba fizikia na sio Fizikia ya ulimwengu" na kuanzia siku hiyo kila alipokuwa akikosea swali mwalimua anamwambia hiyo ni mpemba fizikia na hatimae wanafunzi wakazoea utani huo na kuanza kumtania... Baada ya muda profesa Osborne aliporudi chuoni kwake aliamua kujaribu alicho ambiwa na Mpemba na kikatoa matokea sawa, ndipo walipoanza kuitangaza kwa pamoja na Mpemba mwaka 1969 na kuiandika theori hiyo kwenye majarida, magazeti na vitabu mbali mbali na wakati huo Mpemba alikuwa akisoma chuo cha Afika Wildlife Management (Chuo cha Utawala wa Wanyama Pori) huko mjini Moshi, Kilimanjaro. Na hatimae theori hiyo iliyochukua umaarufu wa jina lake la Mpemba na kuitwa "MPEMBA EFFECT THEORY" na kuwa theori maarufu sana duniani mpaka sasa na hadi sasa mpemba huitwa kwenye mikutano mingi kutoa maelezo ya theori hiyo.

No comments:

Post a Comment